WAKAZI BARINGO WAHIMIZWA KUKUMBATIA AMANI.


Wakazi wa kaunti ya Baringo wamehimizwa kuwa msitari wa mbele kuhakikisha kuwa amani inadumishwa katika maeneo ambayo hushuhudia visa vya wizi wa mifugo.
Kamishina wa kaunti hiyo Henry Wafula amesema kuwa uwepo wa amani kutawapa wanafunzi fursa ya kurejea shuleni na kuendela na masomo yao.
Aidha Wafula amesema kuwepo kwa amani na utulivu kutasaidia pakubwa katika ukuzaji wa kizazi thabiti na kinachoweza kutegemewa na jamii katika siku zijazo.
Wafula amewaonya wakazi ambao wanaedeleza ugemaji na uuzaji wa pombe haramu akisema kuwa watakamatwa na kuchukuliwa hatua kali za kisheria.