WAKAZI 500 KAUNTI YA TURKANA WATARAJIWA KUNUFAIKA NA MIRADI YA MAENDELEO
Zaidi ya wakazi alfu 500 katika kaunti ya Turkana wanatarajiwa kunufaika na miradi mbali mbali ya shilingi milioni 900 zilizotolewa na benki ya dunia.
Miradi hiyo ambayo inatekelezwa chini ya mpango wa Kenya Development Response to Displacement Impact Project inazilenga sekta za afya, maji na vile vile sekta ya elimu.
Miradi hiyo ambayo itagharimu shilingi bilioni 3.2 imefikia awamu ya pili kwa sasa.
Mshirikishi wa mpango huo Thomas Amoni amesema kuwa fedha hizo zitatumika katika kuinua maisha ya wakazi kiuchumi kwa kuwapa ajira na vile vile kuboresha afya zao na viwango vya elimu.
Baadhi ya miradi hiyo imekuwa ikiwanufaisha wakimbizi katika kambi za Kakuma na Daadab.