WAKAAZI WAOMBWA KUWA NA SUBIRA WAKATI MAHAKAMA INAPOENDELEA KUSIKILIZA KESI KUPINGA MATOKEO YA URAIS
Wito umetolewa kwa wakazi wa kaunti hii ya Pokot magharibi kuendelea kuwa na subra wakati mahakama ya juu ikiendelea kusikiliza na hata itakapotoa uamuzi wake kuhusu kesi za kupinga ushindi wa rais mteule William Ruto.
Ni wito wake kamishina katika tume ya kutetea haki za binadam KNCHR Dkt Nyeris ambaye aidha ameeleza imani kwamba jopo la majaji saba wa mahakama ya juu litatoa uamuzi utakaozingatia haki kwa pande zote mbili katika kesi hiyo.
Wakati uo huo Dkt Nyeris ametumia fusa hiyo kuwapongeza wakazi wa maeneo bunge ya Kacheliba na Pokot Kusini kwa kuwa na subira baada ya kuahirishwa chaguzi za ubunge maeneo hayo na hata kushiriki uchaguzi wenye amani.