WAKAAZI WANAMTAKA RAIS WILIAM RUTO KUTEKELEZA YALE ALIYOAHIDI


Wakaazi kutoka kaunti ya Trans nzoia wameendelea kusherehekea kuapishwa kwa Rais Wiliam Ruto wakimuomba kushughulikia changamoto zinazokumba haswa kupanda kwa Gharama ya Maisha.
Wakaazi hao wameendeleza sherehe zao wakifurahia haswa baada ya kuapishwa kwa Rais Wiliam Ruto wakiendelea kumuomba kushughulikia gharama ya maisha ambayo imepanda akisema ameshindwa kuimudu.
Wamemtaka Rais Ruto pia kushughulikia changamoto zinazokumba wafanyibiashara wadogo na kupandishwa kwa gharama ya karo shuleni.