WAKAAZI WA VIHIGA WATISHIA KUVUNJA SERIKALI YA KAUNTI HIYO

Baadhi ya wakaazi katika kaunti ya Vihiga wameanzisha mchakato wa kukusanya saini ili kufanikisha kuvunjwa kwa serikali ya kaunti hiyo.

Kulingana na wakaazi hao ni kwamba serkali ya kaunti hiyo imetumia fedha za umma vibaya kwani miradi yote ya maendeleo iliyoanzishwa haijakamilika.

Aidha wamemsuta gavana Wilber Otichilo kufuatia utumizi mbaya wa ofisi, wizi wa fedha vilevile utoaji wa ajiri bila kufuata utaratibu ufaao

Wakizungumza na wanahabari wakaazi hao wamesema kwamba juhudi zao za kushtaki serkali hiyo zimegonga mwamba kwani gavana Otichilo amekuwa akipuuza maagizo ya mahakama.

Hata hivyo mkurugenzi wa mawasiliano katika ofisi ya gavana Otichilo Victor Wetende amefutilia mbali madai ya wakaazi hao huku akisema kuwa serikali ya kaunti hiyo ii imara.