WAKAAZI WA TUWANI TRANS NZOIA WAPOKEA MWANGAZA BAADA YA KUKAA GIZANI KWA MDA


Wakaazi wa mtaa wa mabanda wa Tuwani kwenye kaunti ya Trans Nzoia sasa wana kila sababu ya kutabasamu baada ya serikali kuekeza katika taa za usalama za usiku, baada ya kukaa gizani kwa miongo mitano.
Wengi ambao wamekuwa wakilazimika kufunga shughuli zao za kibiashara kabla ya giza kuingia sasa wamesema kuwa wataendeleza biashara zao bila kuwa na uoaga.
Hata hivyo akina mama wamesema kuwa wenzao wajawazito na hata wagonjwa ambao wamekuwa wakiathirika zaidi sasa wanaweza kusafiri hata usiku kuelekea hospitalini ili kuhudumiwa.
Benard Wambwa ambaye ni kiranja wa wengi katika bunge la kaunti ya Trans Nzoia hata hivyo ameishukuru serikali kwa kuskiza kilio cha wakaazi wa Tuwani.