WAKAAZI WA SABAOTI WAOMBWA KUJIUNGA NA MRENGO WA AZIMIO LA UMOJA ILIKUWA KATIKA SERIKALI IJAYO


Kiongozi wa kamati ya jamii ya sabaoti ambaye pia alikuwa naibu wa meya mji wa kitale pius arap kauka amepuzilia mbali mrengo wa Kenya kwanza ambao unaongozwa na naibu wa rais wiliam ruto na kinara wa fordkenya moses wetangula na wa anc musalia mudavadi akisema muungano huo hauaminiki
Mzee kauka amesema haifai jamii ya sabaoti kuendelea kuunga mkono mrengo wa Kenya kwanza alipoelezea kuwa vinara wake akiwemo moses masika wetangula hawaminiki akipigia debe mrengo wa azimio na kutaka jamii yake kuunga mkono mrengo huo
Amemkosoa mbunge wa kapseret Oscar sudi kwa kile amedai amekiitaka jamii hiyo kujiunga na mrengo wa Kenya kwanza