WAKAAZI WA POKOT WAHIMIZWA KUDUMISHWA AMANI WAKATI HUU NA BAADA YA UCHAGUZI.

Wito umetolewa kwa wagombea wakisiasa katika kaunti hii ya Pokot magharibi na wakazi kwa jumla kuhakikisha kuwa wanadumisha umoja na utangamano kipindi hiki taifa linapoelekea kwenye uchaguzi mkuu wa mwezi agosti.
Wakiongozwa na Lomery kaperur kutoka wadi ya lomut, wakaazi hao wamekashifu siasa za ukabila na cheche za maneno zinazoendelezwa na baadhi ya wanasiasa ambazo wamesema huenda zitapelekea chuki miongoni mwa waakazi.
Wakati huo huo kaperur ameshtumu kisa cha kushambuliwa kijana mmoja eneo hilo na kuumizwa vibaya katika kisa ambacho kimehusishwa na kampeni za kisiasa akitaka waliotekeleza uovu huo kujitokeza na kuomba msamaha.