WAKAAZI WA POKOT MAGHARIBI WAMTAKA RAIS UHURU KENYATTA KUMTAJA MWIZI ANAYESEMA YUKO SERIKALINI


Hisia mseto zimeibuka miongoni mwa wakazi wa kaunti hii kuhusiana na tamko la Rais Uhuru Kenyatta ya kusema hatamkabidhi mwizi uongozi wa taifa hili atakapotamatisha hatamu yake.
Wakazi hao hasa wanaoumuunga mkono Naibu wa Rais William Ruto wametaka kauli hiyo kutohusishwa kwake huku wengine wakisema wezi ni viongozi wakuu walio serikalini sasa.
Wakazi hao wamemtaka Rais Kenyatta kumtaja mwizi huyo waziwazi na kumchukulia hatua za kisheria iwapo ana ushahidi wa kutosha badala ya kuwapumbaza wananchi ilhali yeye ana mamlaka yote ya kuwachukulia hatua za kisheria wahalifu wote nchini.