WAKAAZI WA ORWO POKOT MAGHARIBI WANUFAIKA NA MRADI WA UNYUNYUZIAJI MAJI MASHAMBA

Na Dismas Terer
Serikali imeendelea kuweka mikakati ya kuhakikisha kuwa wakenya hasa kutoka maeneo kame hawahangaiki kutokana na makali ya njaa ambayo yanachangiwa pakubwa na ukame katika maeneo haya,
Akizungumza katika uzinduzi rasmi wa mradi wa unyunyiziaji maji mashamba wa parasany eneo la Orwo katika kaunti hii ya Pokot magharibi, waziri wa huduma za umma, jinsia na mipango maalum Prof. Margaret Kobia amesema hii ni baadhi ya miradi ambayo serikali inaendeleza kuhakikisha inakabili baa la njaa maeneo haya.
Balozi wa umoja wa ulaya EU ambao ni mmoja wa wafadhili wakuu wa mradi huo Henriette Geiger amesisitiza umuhimu wa amani akisema miradi yoyote ya maendeleo yataafikiwa tu iwapo kutaukuwa na amani katika eneo husika.
Ni kauli ambayo imesisitizwa na gavana wa kaunti hii John Lonyangapuo ambaye pia ametoa wito kwa wahisani zaidi kujitokeza na kuwekeza katika kaunti hii akiwahakikishia uwepo wa usalama wa kutosha kuendeleza shughuli za maendeleo.
Afisa mkuu wa shirika la NRT ambalo limesimamia mradi huo Tom Lalampaa amesema kuwa mradi huo wa miaka minne umefadhiliwa pakubwa na EU kwa yuro milioni 5.4 huku pia akipongeza ushirikiano ambao umetolewa na serikali ya kaunti hii ya Pokot mgharibi.

[wp_radio_player]