WAKAAZI WA MITAA YA MABANDA WAKOSA VYOO VYA UMMA


Uongozi wa kaunti ya Trans Nzoia umetakiwa kujenga vyoo vya umma katika mitaa ya mabanda ya Kipsongo na Matisi ili kuzuia hali ambapo baadhi yao huenda haja katika vichaka karibu na mto Kipsongo.
Wakiongozwa na Fred Munguswa wakaazi hao wameelezea hofu kuwa huenda uchafu huo ukachanganyika na maji wanayoyatumia nyumbani.
Aidha wakazi hao wamesema vichaka hivyo vimeweka watoto wa kike katika hatari ya kudhulumiwa kingono.

[wp_radio_player]