WAKAAZI WA MARIDADI KAUNTI YA TRANS NZOIA WADAI BWENYENYE AMENYAKUA ARDHI YA UMMA YENYE EKARI 20


Wakaazi wa eneo la Maridadi kaunti ya Trans Nzoia wamejitokeza na kuirai serikali ya kitaifa kwa ushirikiano na serikali ya kaunti hiyo kuingilia kati kuhusiana na madai ambayo yamekuwa yakiibuliwa kwamba bwenyenye mmoja amenyakua shamba la umma lenye ekari 20 mablo limejengwa zahanati, shule ya msingi na ya upili ya maridadi.
Kulingana na chifu wa eneo hilo ni kwamba shamba hilo ambalo lilikuwa ni la umma lilinyakuliwa na bwenyenye huyo bila wao kuwa na ufahamu wowote.
Chifu sasa anataka viongozi wa eneo hilo kuingilia kati na kuhakikisha kwamba swala hilo linatatuliwa akisema kuwa hali hiyo inatishia amani katika kijiji hicho.