WAKAAZI WA LORENG’O TURKANA KASKAZINI WAKOSA MVUA KWA ZAIDI YA MIAKA MINNE SASA


Mamia ya wakazi wa eneo la loreng’o, turkana kaskazini wanakabiliwa na hatari ya kuangamia kutokana na ukosefu wa chakula kufuatia kiangazi cha mda mrefu.
Wenyeji eneo hilo wakiongozwa na naibu chufu wa kata ya milima tatu, turkana kaskazini gregory edum na mkazi kwa jina edipo emana wanasema kuwa mara ya mwisho mvua kunyesha eneo hilo ni takriban miaka minne iliyopita.
Wawili hao wanasema kuwa kutokana na kiangazi hicho, wakazi wamekua wakikaa mda mrefu bila chakula na maji huku pia mifugo wakikosa malisho baada ya nyasi kunyauka.
Wenyeji hao wanasema kuwa licha ya kusambaziwa chakula cha msaada na wahisani mbali mbali, watoto wachanga wameendelea kuathirika na tatizo la utapia mlo sawia na akina mama wajawazito.
kauli yao imeunga mkono na sam eledipo ambaye ni afisa wa shirika la save the children.