WAKAAZI WA KAUNTI HII YA POKOT MAGHARIBI WASHAURIWA KUKUMBATIA UKULIMA WA MIMEA


Mshirikishi wa mradi wa kilimo Kenya Climate Smart Philip Ting’aa ameipongeza serikali ya gavana wa kaunti ya Pokot Magharibi Pro John Lonyang’apuo kwa kukumbatia mradi huo ili kuhakikisha kuwa wakulima katika kaunti hii wanawezeshwa.
Akizungumza katika wadi ya Siyoi ambapo wakulima wa eneo hilo walikabidhiwa kondoo zaidi ya 100, Ting’aa amesema kuwa wakulima wengi katika kaunti hii wamenufaika pakubwa kupitia mradi huo.
Wakati uo huo Ting’aa amewahimiza wakulima kuzingatia zaidi upanzi wa mtama pamoja na ndengu mimea anayosema itawanufaisha pakubwa kifedha ikizingatiwa pia inastahimili ukame.