WAKAAZI WA KACHELIBA WANUFAIKA NA MRADI WA MAJI

POKOT MAGHARIBI


Wakazi wa eneo la kamketo kwenye wadi ya kasei wamempongeza katibu katika idara ya ugatuzi kwenye maeneo kame micah powon kwa kuwapokeza mizinga zaidi ya mia mbili ya kisasa pamoja na vifaa vya kutumia wakati wa kurina asali.
Akina mama ambao walikuwa wamewaachia wanaume mradi wa utengenezaji wa mizinga tangu jadi wamekuwa wenye furaha zaidi kwa kukumbukwa na serikali kuu.
Micah powon amewarai wakazi wa eneobunge la kacheliba kwa ujumla kukumbatia mradi huo akisema kwamba asali ya eneo hilo lina umaarufu nchini humu pamoja n amataifa ya nje kutokana na uzuri wake.
Powon aidha amezindua mradi wa uchimbaji wa mabwawa madogo madogo yatakayozisadia familia takriban hamsini kuteka maji ya mvua katika kijiji cha orolwo kwenye wadi ya kodich.
Mradi huo umezinduliwa ili kusuluhisha shida ya uhaba wa maji yanayonywewa na mbuzi, kondoo na ng’ombe katika eneo hilo.