WAKAAZI WA ENEO LA NASOLOT KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI WAPOKEZWA CHAKULA CHA MSAADA


Wakazi wa eneo la Nasolot katika kaunti hii ya Pokot magharibi ambao walipokezwa msaada wa chakula na mahitaji mengine na shirika la msalaba mwekundu kwa ushirikiano na serikali ya kaunti hii wamepongeza shirika hilo kwa msaada huo.

Wakiongozwa na Amos Kemboi Ruto wakazi hao wamesema kuwa wanakabiliwa na wakati mgumu kupata mahitaji ya kimsingi ikiwemo chakula, maji na hata lishe ya mifugo kutokana na ukame ambao umekumba eneo hilo, na hatua hiyo ya msalaba mwekundu ni afueni kwao.

Shirika la msalaba mwekundu ambalo ndilo lililotoa msaada huo limepongeza ushirikiano kutoka kwa serikali za kaunti hii ya pokot magharibi na kaunti jirani ya Turkana kuhakikisha kuwa walengwa wanafikiwa huku likiahidi ushirikiano zaidi kuhakikisha waathiriwa wanasaidika.

Paul Jeling’a ni mwenyekiti wa shirika la msalaba mwekundu eneo hilo.

Hata hivyo viongozi wa kidini eneo hilo wakiongozwa na Daniel Kaporion wametoa wito kwa mashirika zaidi kujitokeza kuwasaidia wakazi hao ambao wengi wao ni waliohama makwano kutokana na visa vya uvamizi hasa maeneo ya mipaka ya kaunti hii na kaunti jirani ya Turkana.