WAKAAZI WA ENEO LA MIPAKANI WATAKIWA KUDUMISHA AMANI


Wakazi wa maeneo ya mipakani pa kaunti hii ya Pokot magharibi na kaunti jirani ya Elgeyo Marakwet, Baringo na turkana wametakiwa kuzingatia amani hasa wakati huu ambapo taifa linaelekea katika uchaguzi mkuu wa mwezi agosti.
Mbunge wa Sigor Peter Lochakapong aidha amewataka wakazi wa maeneo haya kushirikiana na vyombo vya usalama kwa kuwatambua watu wanaoendeleza uvamizi ambao umesabisha wakazi wengi kuyahama makazi yao huku wengine wakipoteza maisha.
Lochakapong amesema kuwa shughuli nyingi muhimu maeneo haya zimekwama kutokana na ukosefu wa usalama huku wakazi wakiendelea kukadiria hasara inayotokana na visa hivyo.
Wakati uo huo Lochakapong amewataka viongozi wa kisiasa eneo la bonde la kerio kuwa makini na matamshi ambayo wanatoa wakati ambapo wanaendeleza kampeni zao za kisiasa kwa ajili ya uchaguzi mkuu ujao na kutotumia lugha ambayo huenda ikasababisha kuvurugwa amani.