WAKAAZI WA ENEO LA KAKONG’ TURKANA KUSINI WALALAMIKIA MAKALI YA NJAA


Zaidi ya wakaazi alfu 12 ambao wanaishi eneo la Kakong Turkana kusini kaunti ya Turkana wanalalamikia makali ya njaa pamoja na ukosefu wa maji kutokana na hali ya ukame ambao umekumba eneo hilo.
Wakazi hao wanasema wanalazimika kutembea mwendo mrefu kutafuta maji hali ambayo pia imepelekea watoto kushindwa kwenda shule kufuatia ukosefu wa bidhaa hiyo muhimu.
Mwakilishi wadi ya Kainuk Lobokat David Rukuli ametoa wito kwa serikali ya kaunti hiyo kuingilia kati ili kuwaokoa wakazi wa eneo hilo.