WAKAAZI WA ENEO LA AMUDAT WATAKIWA KUWA WATULIVU NA KUENDELEZA SHUGHULI ZAO ZA KAWAIDA

Wakazi wa jamii ya Pokot wanaoishi katika wilaya ya Amudat mpakani pa kaunti hii ya Pokot magharibi na taifa jirani la Uganda wametakiwa kuwa watulivu na kuendeleza shughuli zao za kawaida kwa amani eneo hilo.
Akizungumzia utovu wa usalama ambao umeshuhudiwa eneo hilo meya wa mji wa amudat Richard Loru amewataka wakazi jamii ya Pokot kutojihusisha na maswala ambayo huenda yakapelekea utovu wa usalama na badala yake kutumia muda wao kutunza mifugo yao.
Aidha Loru amekosoa vikwazo ambavyo vinawekewa jamii moja eneo hilo dhidi ya kufika maeneo fulani kuendeleza shughuli zao akisema kuwa asheria inawaruhusu kuzuru eneo lolote la taifa hilo muradi wanazingatia sheria na kudumisha amani.
Wakati uo huo Loru amepongeza vikosi vya usalama eneo hilo kwa kuwa msitari wa mbele kuhakikisha kuwa mifugo ambayo imekuwa ikiibwa inarejeshwa, huku akiahidi kuendelea kushirikiana nao kwa ajili ya usalama wa wakazi.