WAKAAZI WA BARINGO WANATAKA JOPO KAZI LILILOTEULIWA KUFIKA MASHINANI KUPOKEA MAONI KUHUSU MTALAA WA CBC

Jopokazi lililoteuliwa na rais dkt william ruto la kutathmini mtaala wa cbc likiwa na kipindi cha miezi sita chaa kusaka maoni kutoka kwa wadau tofauti baadhi ya wakazi kaunti ya baringo wamewataka wanachama wa jopo hilo kuhakikisha kwamba wanapata maoni kamili kutoka kwa wazazi mashinani.

Wakizungumza na kituo hiki wakiongozwa na mkazi kiplimo chepkong’a wanasema kwamba kumekuwa na mazoea ya nyingi za sheria kupasishwa bila kuwahusisha wananchi

Aidha chepkong’a anasema pana haja ya jopo hilo linaloongozwa na prof. Raphael munavu, kuwahusisha watumizi wa mitandao ya kijamii pia kupata maoni kuhusu mtaala wa cbc.