WAKAAZI KAUNTI YA POKOT WAMEHIMIZWA KUTOWABAGUA WATOTO WENYE MIPASUKO KWENYE MIDOMO.


Na Benson Aswani
Jamii katika kaunti hii ya Pokot magharibi imetakiwa kukumbatia watoto wenye tatizo la mipasuko kwenye midomo yani Cleft Clip Palet na kutowatenga kwani ni hali inayoweza kurekebishwa.
Akizungumza baada ya kukamilika zoezi la wiki nzima la kutoa matibabu kwa watu wenye changamoto hiyo katika hospitali ya Kapenguria, mtaalam wa upasuaji ambaye ameongoza shughuli hiyo Dkt Mukami Gathariki amewataka wazazi kutowaficha watoto wenye tatizo hilo na badala yake kuwatoa ili waweze kushughulikiwa.
Amesema kwa ujumla wagonjwa 20 wameshughulikia katika kipindi hicho licha ya kujitokeza zaidi ya wagonjwa 25 akiahidi kurejelewa shughuli hiyo mwezi aprili mwaka 2022 ili kushughulikia wale ambao hawakupata fursa ya kuhudumiwa.
Ni kauli ambayo imetiliwa mkazo na daktari mkuu katika hospitali hiyo ya Kapenguria Dkt David Karuri ambaye amesema kuwa hadi kufikia sasa takriban wagonjwa 70 wamefanyiwa upasuaji tangu kuanza zoezi hilo huku watu 100 wakilengwa katika kipindi cha miaka mitatu tangu mpango huo ulipoanza.
Huyu hapa ni mmoja wa waliopata huduma hiyo kutoka eneo la ziwa kaunti ya uasingishu simion ruto.