WAKAAZI KAKAMEGA WAMTAKA GAVANA OPARANYA KUKAMILISHA MIRADI ALIYOANZISHA


Wakaazi wa kaunti ya Kakamega wamemtaka gavana wao Wycliffe Ambetsa Oparanya kumaliza miradi aliyoianzisha kabla ya hatamu yake ya uongozi kukamilika.
Baadhi ya miradi iliyoanzishwa miaka kadhaa iliyopita ikiwemo ujenzi wa kiwanda cha maziwa malava, hospitali ya Shamakhughu Shinyalu na kiwanda cha majani chai pamoja na nyingine bado hazijakamilika.
Kulingana na mwenyekiti wa muungano wa wakaazi wa kaunti hiyo Patrick Wabuku, wanataka miradi hiyo kutekelezwa kikamilifu na pia sekta za afya, kilimo na miundo msingi kuimarishwa.
Ni kauli ambayo seneta wa Kakamega Cleophas Malala amekuwa pia akishinikiza.
Ikumbukwe ni wiki jana tu ambapo Gavana Wycliffe Oparanya aliwaagiza mawaziri wake kusitisha miradi yote mpya ili kukamilisha miradi ambayo imekwama kabla ya mwisho wa mwaka huu.