WAKAAZI ENEO LA SIGOR WAOMBWA KUDUMISHA AMANI WAKATI HUU WA UCHAGUZI
Wito umetolewa kwa wakazi wa kaunti hii ya pokot magharibi kudumisha amani na kutokubali kutumika vibaya na wanasiasa kuvuruga amani kwa manufaa yao ya binafsi hasa wakati huu ambapo taifa linakaribia uchaguzi mkuu wa tarehe 9 mwezi agosti.
Ni wito wake mgombea kiti cha ubunge eneo bunge la sigor philip rotino ambaye amewataka wakazi kuwa makini na kuwapiga msasa wagombea wa nyadhifa za kisiasa ili kuwachagua viongozi wenye maadili na wenye rekodi bora ya maendeleo.
Ni kauli ambayo imetiliwa mkazo na seneta wa kaunti hii samwel poghisio ambaye amewataka wanasiasa kaunti hii kuendesha kampeni zao kwa njia inayokubalika kisheria na kutowatumia vijana kwa malengo yao ya kibinafsi, huku akitishia kuwataja wazi wanasiasa anaodai kuwa wanawatumia vijana kuvuruga amani iwapo wataendelea na tabia hiyo.
Aidha rotino amewataka wanasiasa kutozungumzia maswala ya mipaka wanapokua kwenye majukwa ya kisiasa ili kuepuka uhasama na kaunti jirani.