WAJANE NA MAYATIMA KUTOKA ENEO BUNGE LA LURAMBI KAUNTI YA KAKAMEGA WAPOKEA MSAADA WA KIFEDHA ILI KUANZISHA BIASHARA


Kanisa la Holy Apostolic Believers Church kaunti ya Kakamega limeanzisha mradi wa kuwapa vyakula na fedha wajane na mayatima kutoka eneo bunge la Lurambi ili kuanzisha biashara, ambao wamejitoza kwenye bahari la ugemaji wa pombe haramu ya chang’aa.
Akiongea wakati wa kutoa msaada wa vyakula kwa zaidi ya wajane 100 na mayatima katika mtaa wa Shirere, mmoja wa viongozi wa kanisa hilo amesema mpango huo unalenga kuwang’amua wahusika kutoka minyororo ya utengenezaji wa pombe na uuzaji wa mihadarati akitaka serikali kuwaorodhesha kwenye mpango wa marupurupu ya kila mwezi kwa wakongwe.
Walionufaika na msaada huo chini ya Marceline Bahati hata hivyo wametoa shukrani zao na kuwataka wahisani zaidi kujitokeza na kuwasaidia.