WAHUDUMU WA UCHUKUZI WA UMMA WACHANGAMKIA ASILIMIA 100 YA ABIRIA.


Hisia mseto zimeendelea kuibuliwa miongoni mwa wananchi baada ya serikali kuruhusu asilimia 100 ya abiria katika sekta ya uchukuzi wa umma nchini.
Wakiongozwa na meneja wa magari ya sacco ya Kitale- Kapenguria John Pusia, wahudumu wa magari mjini Makutano kaunti hii ya Pokot magharibi wamepongeza hatua hiyo wakiahidi kuzingatia kikamilifu maagizo ya wizara ya afya katika kukabili maambukizi ya corona.
Aidha wamesema kuwa nauli itapunguzwa hadi ilipokuwa awali kabla ya kuanza janga la corona ili pia kuleta afueni kwa wateja wao.
Wakati uo huo Pusia ametoa wito kwa serikali kuruhusu kurejelewa safari za usiku ili kuwawezesha kulipia mikopo wanayodaiwa kwani wamehangaika pakubwa tangu ujio wa janga la corona nchini.
Hata hivyo baadhi ya wahudumu hao pamoja na wakazi wa kaunti hii wametofautiana na agizo hilo wakisema kuwa kujaza watu kwenye magari kutepelekea kusambaa zaidi virusi vya corona kutokana na hali kuwa takwa la umbali kutoka mtu mmoja hadi mwingine halitazingatiwa.