WAHUDUMU WA MATATU MJINI KITALE WALALAMIKIA UKOSEFU WA VYOO KATIKA KITUO KIKUU CHA MABASI CHA KITALE


Uhaba wa vyuo vya kutosha na maji safi mjini Kitale umewasababishia wasafiri, wafanyibiashara na wahudumu wa magari ambao wanahudumu katika kituo kikuu cha mabasi cha kitale kuhangaika pakubwa wanapoendeleza shughuli zao.
Wakiongozwa na mwenyekiti wa wahudumu wa magari ya uchukuzi Simon Andala wahudumu hao wamesema kuwa ni choo kimoja tu ambacho kinawashughulikia wasafiri zaidi ya elfu 3 ambao wanatumia kituo hicho kila siku.
Andala ameongeza kuwa hali hiyo huenda ikasababisha magonjwa kwa wale ambao wanakitumia huku wakitaka serikali ya kaunti hiyo chini ya G avana Patrick Khaemba kuingilia kati.
Wakati uo huo wahudumu hao wamesema kuwa msongamano mkubwa unashuhudiwa kutokana na wachuuzi ambao wanafanya shughuli zao kando kando mwa bara bara za kituo hicho.