WAHUDUMU WA MAGARI WALALAMIKIA VIZUIZI VYA POLISI ORTUM.


Wahudumu wa magari ya uchukuzi ya kutoka mjini makutano kuelekea ortum kaunti hii ya pokot magharibi wamelalamikia vizuizi vingi vya polisi ambavyo vipo kwenye barabara hiyo wakitaka idara husika kuvipunguza.
Wakiongozwa na Samson Kautich, wahudumu hao wamesema kuwa uwepo wa vizuizi hivyo unawapelekea kutumia fedha nyingi wanazoitishwa na maafisa wa trafiki hali ambayo inawafanya kutoafikia malengo yao mwisho wa siku.
Wakati uo huo wahudumu hao wamelalamikia kukithiri utovu wa usalama eneo la ortum hali ambayo imechangiwa na kukithiri ugemaji pombe pamoja na vijana kuingilia michezo ya karata nyakati za usiku wakitaka wakuu wa usalama eneo hilo kushughulikia hali hiyo.