WAHUDUMU WA BODA BODA WATAKIWA KUWA MAKINI DHIDI YA WIZI WA PIKIPIKI.
Vijana katika kaunti hii ya Pokot magharibi wanaonunua pikipiki na kujiunga na sekta ya boda boda wametakiwa kuwa waangalifu na kuchukua tahadhari dhidi ya wizi wa pikipiki ambao umeripotiwa kuongezeka katika kaunti hii.
Ni wito wake waziri wa biashara na viwanda kaunti hii Francis Kitalawian ambaye aidha ametoa wito kwa idara za usalama kuhakikisha kuwa visa vya wizi wa pikipiki vinakabiliwa ili kuhakikisha usalama wa wahudumu hao.
Aidha Kitalawian amewahimiza vijana waliopokezwa pikipiki kupitia sacco ya wepesa kujiunga katika makundi mbali mbali yanayopatikana kwenye kaunti hii ili kuimarika zaidi katika biashara hiyo na kujiendeleza kiuchumi.