WAHUDUMU WA BODA BODA WATAKIWA KUHUBIRI AMANI POKOT MAGHARIBI.

Wahudumu wa boda boda katika kaunti hii ya Pokot magharibi wametakiwa kutumia nafasi yao kuhubiri amani msimu huu wa siasa za uchaguzi mkuu wa mwezi agosti ili kuhakikisha kuwa uchaguzi huo unaandaliwa katika mazingira ambayo yatawaruhusu kuendelea na shughuli zao bila kuathirika.
Akizungumza wakati wa kikao na wahudumu hao, mwenyekiti wa vijana youth bunge kaunti hii Richard Todosia amewataka wahudumu hao pia kutokubali kutumika na wanasiasa kuvuruga amani kwa maslahi yao ya kibinafsi.
Wakati uo huo Todosia ambaye pia ni mgombea kiti cha mwakilishi wadi ya Mnagei kwa tiketi ya chama cha UDA amesema kuwa uongozi wake utatoa kipau mbele kwa maendeleo ya vijana na akina mama akiahidi uongozi bora katika kipindi chake iwapo atachaguliwa.