WAHUDUMU WA BODA BODA WANAOSHIRIKIANA NA WEZI WAONYWA MALAVA KAKAMEGA


Onyo kali imetolewa kwa wahudumu wa boda boda ambao watashirikiana na wahalifu kutekeleza visa vya kihalifu nyakati za usiku eneo la Malava kaunti ya Kakamega kwamba watakabiliwa ipasavyo.
Ni onyo ambalo limetolewa na mwenyekiti wa muungano wa wahudumu wa boda boda eneo la Malava Chitunga Museve ambaye amesema kuwa wamepokea ripoti kwamba baadhi ya wahudumu hao wanashirikiana na wezi kutekeleza wizi nyakati za usiku.
Wakati uo huo Museve amewaonya wahudumu wa boda boda eneo hilo ambao wana hulka ya kuwaandama wanafunzi na kujihusisha nao kimapenzi kuwa hawatawavumilia kwani wanaharibia sifa sekta hiyo kwa jumla.