WAHUDUMU WA BODA BODA WALALAMIKIA KUHANGAISHWA NA ASKARI WA KAUNTI MJINI MAKUTANO POKOT MAGHARIBI.

Na Benson Aswani
Baadhi ya wahudumu wa boda boda katika kaunti hii ya Pokot magharibi wanalalamikia jinsi askari wa kaunti mjini makutano wanavyotekeleza majukumu yao.
Wakiongozwa na Paul Lonapa wahudumu hao wamesema kuwa wamekuwa wakihangaishwa na maafisa hao na kutozwa fedha nyingi pikipiki zao zinaponaswa na maafisa hao kutokana na madai ya kutozingatia sheria za kuegesha pikipiki hizo mjini Makutano.
Wametoa wito kwa uongozi wa kaunti hii kuwapa maafisa hao mwongozo wa kutekeleza majukumu yao ili kuwazuia kutumia nafasi zao kuwanyanyasa wahudumu hao.