WAHUDUMU WA AFYA KATIKA HOSPITALI YA SABOTI WANAFANYA KAZI KWENYE MAZINGIRA DUNI


Mwenyekiti wa chama cha wafanyikazi katika kaunti ya Trans Nzoia Samwel Kiboi ameishtumu serikali ya kaunti kufuatia mazingira duni ya kufanyia kazi katika hospitali ya Sabaoti kwenye kaunti hiyo.
Akizungumza na wanahabari Kiboi amehoji kwamba wahudumu wa afya hawana vifaa vya matibabu hali inayolemaza kabisa utoaji huduma kwa wagonjwa.
Kiboi ameongeza kuwa wahudumu hao wako kwenye hatari ya kuambukizwa virusi vya corona iwapo serkali hiyo haitazingatia masilahi yao.
Amesema kwamba ilivyo sasa wahudumu hao hawana maski na vifaa vya kupima virusi vya corona
Kadhalika amehoji kwamba hospitali hiyo haina ambulensi ya kuwasafirisha wagonjwa wanaohitaji matibabu ya dharura
Kiboi ameilamu wizara ya afya kwenye kaunti kufuatia utepetevu huo.