WAHISANI ZAIDI WA SEKTA YA KILIMO WATAKIWA KUJITOKEZA KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI.


Waziri wa kilimo na mifugo katika kaunti hii ya Pokot magharibi Geofrey Lipale amewapongeza wahisani ambao wamejitokeza katika kaunti hii kupiga jeki juhudi za wakulima hasa kupitia shughuli ya kutoa chanjo kwa mifugo dhidi ya magonjwa mbali mbali.
Lipale amesema kuwa hatua hii itapelekea kuimarika uchumi wa wakulima kwa kuwahakikishia usalama wa mifugo yao akitoa wito kwa wahisani zaidi kujitokeza na kuwafaa wakulima.
Wakati uo huo Lipale ametoa wito kwa wakulima katika kaunti hii kushirikiana vyema na wahisani hao kwa kuwaleta mifugo yao kupokea chanjo katika maeneo ambako shughuli hiyo inaendelea, akisema kuwa chanjo zote zinazotolewa ni salama kwa mifugo.