WAHISANI WATAKIWA KUWASAIDIA WANAFUNZI WALIOKOSA UFADHILI WA ELIMU SCHOLARSHIP BARINGO.


Wahisani mbalimbali katika kaunti ya baringo wameshauriwa kushirikiana kwa pamoja ili kuhakikisha watahiniwa zaidi ya 700 ambao hawakupata fursa ya kujiunga na shule za upili kupitia mradi wa elimu scholarship wamepata usaidizi na kutimiza ndoto zao maishani.
Akiongea mjini kabarnet wakati wa uzinduzi wa mpango wa elimu scholarship ambapo watahiniwa 46 pekee waliteuliwa kati ya 800 waliotuma maombi, meneja wa benki ya equity, micah bett ambaye alisimamia uteuzi huo amebainisha kuwa 46 waliochaguliwa walikuwa na uhitaji mkubwa.
Bett hata hivyo amedokeza kuwa maeneo bunge ya baringo kusini na tiaty yalikuwa na mahitaji mengi ila nafasi zilizotolewa hazikutosha.