WAGONJWA WA KISUKARI TRANS NZOIA WATAKIWA KUJITOKEZA KUPATA MATIBABU.

Na Benson Aswani
Kaunti ya Trans nzoia imerekodi idadi ya watu alfu nne wanaougua ugonjwa kisukari huku wito ukitolewa Kwa wakazi wanaougua ugonjwa huo kutembelea vituo vya afya ili kupata matibabu.
Kwa mujibu Wa waziri wa afya Kaunti ya Trans nzoia Clare wanyama idadi hii ni kubwa mno na ipo haja ya wagonjwa wa kisukari Kujitokeza na kupokea matibabu ili kukabili ugonjwa huo.
Kwa upande wake Silas Wambulwa Daktari na msimamizi wa matibabu ya magonjwa sugu Kaunti ya Trans Nzoia amesema ukosefu wa mazoezi na pia mazoea ya kula wa chakula kilicho na wanga kwa wingi ndio chanzo cha hali hiyo inayoambatana na shinikizo la damu.
Ni kauli iliyoungwa mkono na Catherine Njogu mtaalam wa lishe bora akirai wananchi kufanya vipimo vya mara kwa mara mbali na kutafuta huduma za afya mapema ili kujiepusha madhara zaidi.