WAGONJWA KATIKA HOSPITALI YA LEVEL MJINI KITALE KUNUFAIKA NA MSAADA WA CHAKULA.


Zaidi ya wagonjwa 7,500 katika Hospitali kuu ya level four mjini Kitale wanatarajiwa kunufaika na msaada wa chakula kutoka kwa shirika la Visa oshwal community mjini Kitale wa kima cha shilingi laki moja kwa muda wa siku kumi zijazo.
Akihutubu wakati wa kupokea vyakula hivyo waziri wa afya Kaunti ya Trans Nzoia clare wanyama amepongeza hatua hiyo akisema itasaidia katika kupiga jeki lishe bora mbali na kuonyesha utu kwa wagonjwa wanaoendelea na matibabu kwenye hospitali hiyo.
Ni matamushi yaliotiliwa mkazo na afisa mkuu katika wizara ya afya Kaunti ya Trans-Nzoia Charlse Baraza akisema kwa siku kumi sasa shirika la visa Oshawal limekuwa likisaidia katika kutoa msaada huo wa chakula kwa hopitali hiyo akisema chakula ni kiungo muhimu katika utoaji wa matibabu kwa wagongwa walio lazwa.