WAGOMBEZI HURU WASHAURIWA KUJA PAMOJA NA KUTATUA MGOGORO UNAOWAKUMBA ENEO LA ENDEBES KAUNTI YA TRANSNZOIA

Wazee wa jamii ya luhya eneo bunge la endebes kaunti ya transnzoia wameanzisha mikakati ya kuwaweka pamoja wagombezi huru eneo hilo ilikupata mwaniaji mmoja mwenye umaarufu ilikuimarisha nafasi yao ya kushinda agosti tisa
Hatua hii inajiri kufuatia masikitiko ya mchujo wa chama cha dapk baada ya zoezi la mchujo kutofanyika na badala yake uongozi wa chama hicho kuamua kuwakabidhi baadhi ya wawaniaji vyeti vya moja kwa moja na hivyo kuwalazimu wengine wao kujisajili kama wagombea huru
Lengo sasa la wazee hao ni kuelekeza jamii hiyo kuhusu ni nani wanayepaswa kuunga mkono
Wanasema iwapo watafumbia macho suala hilo huenda mrundiko wa wagombea huru kwenye nyadhifa mbalimbali eneo hilo ikainyima jamii ya luhya nafasi ya uongozi
Amesimulia kuwa eneo hilo limesalia nyuma kimaendeleo kutokana na uongozi wa vyama kuwalazimishia viongozi kila mara suala ambalo wanajutia na sasa wanasema wako tayari kujikomboa.