WAGOMBEA WA UDA KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI WALIOSHIRIKI MCHUJO WAMEPINGA MATOKEO HAYO

Baadhi ya wagombea wa chama cha UDA walioshiriki mchujo wa chama hicho katika kaunti hii ya Pokot magharibi wamedai zoezi hilo hali kuandaliwa kwa njia ya haki.
Mwakilishi wadi yaMnagei anayeoondoka Benjamin Araule amedai kuwa baadhi ya maafisa waliosimamia zoezi hilo wali onyesha wazi kuwapendelea baadhi ya wagombea hali iliyopeleka wagombea wengine kutendewa hujuma.
Araule amedai kuwa kura ziliibwa kwenye mchujo huo kwa kumpendelea mgombea ambaye alishinda kwenye zoezi hilo Richard Todosia.
AidhaAraule amepuuzilia mbali uwezekano wakuwania tena kiti hicho kama mgombea huru katika uchaguzi mkuu wa mwezi agosti akisema kuwa atatumia muda wake kutekeleza shughuli zake za kibanfsi ilikumpa nafasi atakayechaguliwa katika uchaguzi huo kuwahudumia wakaazi.