WAGOMBEA VITI VYA KISIASA POKOT MAGHARIBI WATAKIWA KUJITOKEZA WAZIWAZI.


Baadhi ya wakazi wa kaunti hii ya Pokot magharibi wamewataka viongozi wote ambao wanaazimia kuwania kiti cha useneta kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka ujao kujitokeza na kutangaza wazi azma yao ili kutoa mwelekeo halisi wa kinyang’anyiro hicho.
Wakiongozwa na Chemichich Limakit wakazi hao wamesema kuwa wapo baadhi ya wanaoazimia kugombea kiti hicho kando na seneta wa sasa Samwel Poghisio na Julius Murgor ila hawajatangaza rasmi, sasa wakiwataka kujitokeza waziwazi ili kubaini mkondo halisi wa siasa za kaunti hii.
Wakati uo huo Limakit ambaye ni mmoja wa wanaharakati katika kaunti hii ya Pokot magharibi amepuuzilia mbali chama kipya kinachobuniwa kaunti hii akiwataka wakazi kuunga mkono vyama ambavyo vitawapa sauti katika ngazi ya kitaifa.