WAGOMBEA VITI MBALIMBALI KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI WAMEHAKIKISHIWA MCHUJO WA HURU NA WA HAKI
Wagombea nyadhifa za kisiasa kupitia chama cha UDA Kaunti hii ya Pokot magharibi wameelezea imani ya kuandaliwa mchujo ulio huru na wa haki.
Mgombea kiti cha ubunge eneo la Pokot kusini Joel Arumonyang amesema kuwa chama hicho kimew eka mikakati ya kutosha kufanikisha shughuli hiyo itakayoandaliwa tarehe 14 mwezi aprili wakipata hakikisho la uwazi wa shughuli hiyo kutoka kwa kiongozi wa chama naibu rais William Ruto.
Arumonyang ameelezea imani ya kuibuka mshindi katika mchujo huo wa chama na kisha kupeperusha bendera ya chama hicho eneo bunge la Pokot kusini kwenye uchaguzi mkuu wa mwezi agosti hasa baada ya utafiti kuashiria ndiye aliye kifua mbele miongoni kwa wagombea wa chama cha UDA.
Kwa upande wake mgombea kiti cha mwakilishi wadi ya Tapach Veronica Long’ole amewataka wafuasi wa chama cha UDA kujitokeza kwa wingi siku hiyo kuwachagua wagombea watakaomenyana na wagombea wa vyama vingine.