WAGOMBEA VITI KWA CHAMA CHA DAP K WAMEKOSA AMANI NA MCHUJO ULIOKAMILIKA TRANSNZOIA KAUNTI


Wagombea viti vya ubunge katika chama cha DAP K wanazidi kutoa lalama zao kuhusu kutoandaliwa kwa kura ya mchujo kwa chama hicho licha ya kulipia ada ya zoezi hilo wakidai kwamba chama hicho kimewatapeli.
Wakiongzwa na Jami Simiyu mgombea kiti cha eneo bunge la Endebess na Amos Wanjala mwakilishi Jacob Nasongo mgombezi wa kiti cha eneo bunge la Kwanza wanadai kwamba baadhi ya wagombea wenza wamepewa tiketi ya moja kwa moja bila hata mashauriano miongoni mwa wagombea viti hivyo,wakitaka kujua ni vigezo gani vilivyotumika na chama hicho kutoa tiketi hizo kwa wagombea hao.
Hatua ya chama hicho kinachoongzwa na mbunge wa Kanduyi Wafula Wamunyinyi imewagadhabisha baadhi ya wapiga kura eneo la Chepchoina eneo bunge la Endebess wakimtaka waziri wa ulinzi Eugine Wamalwa kuingilia kati la sivyo kukigura chama hicho na kuwapigia kura wagombea huru kwenye kinyanganyiro cha Agosti 9.