WAGOMBEA NYADHIFA ZA KISIASA WAPONGEZWA KWA KUWATEUA WANAWAKE KUWA WAGOMBEA WENZA.
Hatua ya Viongozi mbali mbali kuwateua akina mama kuwa wagombea wenza nchini inazidi kupokelewa vyema na baadhi ya Viongozi katika Kaunti ya Trans-Nzoia.
Mgombea wa kiti Cha ubunge eneo la Endebess kwa chama cha ODM Moses masinde amewarai akina mama kujitokeza na kuwania nyadhifa mbali mbali za uongozi ,akiwapongeza baadhi ya Viongozi nchini kuwateua akina mama hao Kama wagombea wenza.
Masinde amesema hatua hiyo inaliweka taifa la Kenya kuwa miongoni mwa mataifa yanayowahusisha akina mama Katika masuala ya uongozi.