WAFUASI WA UDA WACHANGAMKIA ZIARA YA NAIBU RAIS POKOT MAGHARIBI.


Naibu rais William Ruto anapotarajiwa kuzuru kaunti hii ya Pokot magharibi kuendeleza kampeni zake za hustler nation wafuasi wa chama cha UDA katika kaunti hii wameelezea utayarifu wa kumpokea kiongozi huyo punde atakapowasili.
Wakitolea hisia ziara hiyo ya ruto wakazi hao wameitaka idara ya usalama kuhakikisha kuwa kunakuwa na usalama wa kutosha naibu rais atakapowasili huku wakielezea imani ya ufanisi mkubwa wa ziara hiyo kwa madai kuwa eneo hili ni moja ya ngome kuu za chama cha UDA.
Wametoa wito kwa wafuasi wa chama cha UDA kutoka maeneo mbali mbali ya kaunti hii ya Pokot magharibi kujitokeza kwa wingi ili kumpokea Ruto.