WAFUASI WA UDA POKOT MAGHARIBI WAVUNJA KIMYA CHAO KUHUSU KUTIMULIWA CALEB KOSITANY KUTOKA KWA CHAMA CHA JUBILEE


Wafuasi wa chama cha UDA kichohusishwa na naibu wa rais William Ruto katika kaunti hii ya Pokot Magharibi wametoa hisia zao kuhusiana na kutimuliwa kwa Caleb Kositany kutoka kwenye Chama cha Jubilee.
Kulingana nao, rais Uhuru Kenyatta amefanya hayo ili kumkasirisha naibu wake baadaye apate kigezo kamili cha kutengana naye licha ya maagano yao kwenye uongozi.
Wamesema kutimuliwa kwa wendani wa Ruto kutamzidishia umaarufu nchini kinyume na matarajio ya wanaomchukia.
Wakati uo huo wafuasi wa chama cha ODM wametaka kinara wao Raila Odinga asihusishwe kivyovyote kwenye malumbano ya chama cha Jubilee.