WAFUASI WA ODM TRANS NZOIA WAHIMIZA AMANI KATIKA MKUTANO WA BUKHUNGU 2.


Wafuasi wa chama cha ODM Kaunti ya Trans Nzoia wamewarai vijana kutoka magharibi ya nchi kuhubiri amani katika Mkutano wa Bukhungu hii leo wakisema Francis Atwoli na Gavana wa Kakamega Wycliffe Oparanya wanafaa kuheshimiwa na hivyo vitisho vya Malala havitawazuia wananchi kuhudhuria mkutano huo.
Wakiongozwa na Brian Khisa wafuasi hao wa ODM wamewataka wananchi kuelekea Bukhungu hii leo huku wakipuuzilia mbali matamushi ya Seneta wa kakamega Cleophas Malala kuhusu mkutano huo waliyoyataja kuwa uchochezi.
Wakati uo huo wamewataka vijana kuepuka kutumiwa vibaya na wanasiasa wanaojitakia makuu wakidai Seneta Malala ni Kibaraka wa Naibu wa Rais William Ruto.

[wp_radio_player]