WAFUASI WA DAP-K TRANS NZOIA WATAKA WASHINIKIZA UWAZI KATIKA ZOEZI LA UTEUZI.


Wafuasi na wawaniaji wa chama cha Democratic Action Party of Kenya (DAP-K) Kaunti ya Trans Nzoia wamewarai viongozi wa chama hicho kuhakikisha kwamba shughuli ya mchujo katika chama hicho inaendeshwa kwa uwazi.
Wakiongozwa na Lenox Juma anayewania kiti cha Wadi ya Matisi wanachama hao wamesema uwazi katika kura ya mchujo utapelekea chama hicho kupata viti vingi kwenye uchaguzi mkuu ujao kwani utaongeza uaminifu wa wanachama kwa chama hicho.
Aidha Juma amewataka wakazi wa Matisi ambao hawana kura kujisajili ili kupata nafasi ya kuwachagua viongozi bora Agosti tisa huku akisuta uongozi mbaya ulioko kwa sasa ambao umeshindwa kuwasaidia wananchi ipasavyo.

[wp_radio_player]