WAFANYIKAZI TRANS NZOIA WATISHIA KUGOMA KULALAMIKIA KUCHELEWESHWA MSHAHARA.


Mwenyekiti wa muungano wa wafanyakazi wa serikali ya Kaunti ya Trans Nzoia Samuel Juma Kiboi ametoa makataa ya siku tatu kwa serikali ya Kaunti hiyo kuwalipa mishahara yao ya miezi mitatu la sivyo washiriki mgomo.
Kwenye mkao na wanahabari mjini Kitale Kiboi anadai kwamba wafanyakazi Kaunti hiyo wanaendelea kupitia hali ngumu maishani kutokana na ukosefu wa mishahara kwa miezi mitatu sasa huku wakihitajika kuwalipia wanao karo mbali na mahitaji mengine ya kimsingi kumudu maisha.
Aidha Kiboi anasema serikali ya Kaunti ya Trans Nzoia imefeli kwenye usimamizi wa wafanyakazi wake jambo linalopelekea utendaji kazi duni katika usimamizi na utekelezaji wa miradi mingi ya maendeleo hivyo kuchangia kukwama miradi hiyo.