WAFANYIBISHARA BUNGOMA WALALAMIKIA KUTOPATA FEDHA ZILIZOTOLEWA NA NAIBU RAIS.

Na Benson Aswani
Viongozi wa wafanyibiashara katika soko la Chepkube mjini Bungoma wanadai maisha yao yamo hatarini baada ya wenzao kuwashuku kuwa huenda wanafahamu zilipo pesa ambazo naibu rais William Ruto aliyeahidi kuwapa wafanyibiashara wadogo wadogo katika soko hilo kuwapiga jeki katika biashara zao alipozuru kaunti ya Bungoma juma lililopita.
Wakiongozwa na mwenyekiti wa wafanyibiashara hao Benard Makokha, viongozi hao wamesema kuwa wamelazimika kupiga ripoti kwa kituo cha polisi baada ya baadhi ya wafanyibiashara kusemekana kuwatembelea nyumbani mwao huku wakitaka kupewa mgao huo wa pesa.
Wafanyibiashara hao sasa wanamtaka naibu rais William Ruto kuweka wazi swala hili ili waweze kubaini kilichojiri baada ya yeye kuahidi kuwapa fedha hizo kuinua biashara zao jinsi alivyofanya maeneo mengine ambayo amezuru nchini.