WAFANYIBIASHARA WATISHIA KUANDAMANA KUTETEA BIASHARA ZAO MAKUTANO.


Wafanyibiashara mjini Makutano katika kaunti hii ya Pokot magharibi wametishia kuandamana hadi afisi ya mkurugenzi wa elimu kaunti hii kulalamikia hatua ya uongozi wa baadhi ya shule katika kaunti hii kuingilia biashara zao.
Wafanyibiashara hao wamesema kuwa biashara zao ziliathiriwa pakubwa na janga la corona na hatua ya baadhi ya shule kuwauzia wanafunzi wanaosajiliwa kujiunga na kidato cha kwanza bidhaa zinazohitajika ni kuhujumu shughuli zao ikizingatiwa wao hunufaika mara moja kwa mwaka.
Wakiongozwa na Mark Loriso naibu mwenyekiti wa chama cha wafanyibiashara chamber of commerce tawi la pokot magharibi, wafanyibiashara hao sasa wanatoa onyo kwa wakuu wa shule dhidi ya kuhusika na biashara zao akisema kuwa watashinikiza kuchukuliwa hatua dhidi ya shule ambayo itapatikana ikiendesha biashara hizo hata ikibidi kufungwa.