WAFANYIBIASHARA WATAKIWA KUIMARISHA USAFI MJINI MAKUTANO.


Wafanyibishara mjini makutano katika kaunti hii ya Pokot magharibi wametakiwa kushirikiana na serikali ya kaunti katika kuhakikisha kuwa usafi unadumishwa maeneo yao ya kazi.
Akizungumza baada ya kuongoza shughuli ya kusafisha mji wa makutano, msimamizi wa idara ya afya eneo la Kapenguria Musa Barasa anesena kuwa licha ya kuwa ni jukumu la serikali kuhakikisha mazingira salama ya wafanyibiashara ni jukumu la wafanyibiashara hao pia kuhakikisha usafi wa eneo wanakofanyia kazi.
Kwa upande wake afisa katika wizara ya afya kaunti hii kitengo cha usafi wa mazingira Abel Koech amesema shughuli hiyo inatarajiwa kuendelezwa hadi maeneo ya mashinani ambapo inazinduliwa rasmi leo huku akielezea matumaini ya mashirika mbali mbali yasiyo ya serikali kushirikiana na serikali ya kaunti katika zoezi hilo.